Spika Mstaafu wa Bunge, Anne Makinda amesema ni muda wa kuweka ukomo kwa Wabunge wa Viti Maalum kwakuwa sio sawa kwa wenye nafasi hizo kwa muda mrefu.
Amesema utaratibu wa Viti Maalum ulianzishwa kwa ajili ya kuwaandaa Wanawake kugombea Majimboni lakini wanaoshikilia nafasi hizo kwa muda mrefu wamekuwa wakiwanyima fursa Wanawake wengine.
Ameeleza kuwa upatikanaji wa Wabunge hao katika baadhi ya Vyama vya Siasa ni wa mashaka na inahuzunisha ukifuatilia jinsi walivyopata vyeo hivyo.