Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe amepokea vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni 22 kutoka kwa Doris Mollel aliyewahi kuwa Miss Tanzania namba 3 2014 ambaye kwa sasa anafanya kazi na foundation yake aliyoianzisha 2015 inayojihusisha na kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti).
Doris Mollel kupitia foundation yake hiyo ametoa msaada kwa Hospital ya Wilaya ya Handeni baada ya kugundua kuwa wazazi wanaojifungua kabla ya wakati wamekuwa wakipewa rufaa ya kwenda kupewa huduma Hospitali ya Bombo na zingine kwa umbali mrefu kitu ambacho kinachangia na kuhatarisha maisha ya Mtoto huyo.
Awali wazazi waliokuwa wakijifungua watoto kabla ya wakati ( Njiti ) walikuwa wakipelekwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga ambayo ni umbali wa kilometer 160 kutoka Wilaya ya Handeni.