Leo March 11, 2020 Waziri wa Afya wa Uingereza, Nadine Dorries amepatikana na maambukizi ya Virusi vya Corona na anakuwa Mbunge wa kwanza Uingereza kuathirika na mlipuko huo.
Waziri huyo amesema alifuata tahadhari zote zilizotolewa baada ya kugundua ameambukizwa na amejiweka karantini nyumbani tangu Ijumaa huku afya yake ikiendelea vizuri.
Taarifa zilizotolewa na Wizara ya Afya zinasema Dorries alianza kuonesha dalili za Corona Virus wiki iliyopita, siku ambayo alihudhuria tukio lililoandaliwa na Waziri Mkuu.
Mawaziri wote wa Afya pamoja na viongozi wengine waliokuwa karibu na Waziri Dorries wametakiwa kufanya vipimo kuangalia kama wameambukizwa.
Watu 6 wamefariki dunia kutokana na Corona Uingereza na idadi ya walioambukizwa Virusi hivyo imefikia 382.