Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Mkami Shirima mkazi wa Ilikiurei, Arusha, anadaiwa kumuua mfanyakazi wake wa ndani Salome Zacharia kwa kumpiga fimbo akimtuhumu kuiba Tsh.Elfu 50.
Mwanamke huyo ambae anashikiliwa na Polisi Arusha, anadaiwa kutenda tukio hilo Alhamisi wiki iliyopita na baadae alimfungia katika chumba kimoja nyumbani kwake kwa muda wa siku mbili bila kumpatia chakula wala maji ya kunywa huku akimcharaza fimbo hadi kupelekea kifo chake.