Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Festo Maduhu, Mkazi wa Mtaa wa Benki Kabwe Jijini Mbeya kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake na kisha yeye mwenyewe kujaribu kujiua kwa kisu.
Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ulrich Matei amesema tukio hili limetokea jana, huku kiini cha tukio hilo kikielezwa kuwa ni wivu wa mapenzi, a,mbapo Maduhu alikuwa akimtuhumu mwenzake kuwa ana mahusiano na mwanaume mwingine.
“Ni kwamba Machi 23, 2020, majira ya saa 09:00 asubuhi, huko katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Negero, iliyopo Mtaa wa Ilolo, Kata ya Ruanda, katika chumba namba 111, mwanamke mmoja aitwaye Jesca Michael, Mhudumu wa nyumba ya kulala wageni na bar, aligundulika kuuawa kwa kukabwa shingo na kupigwa sehemu za usoni na mtuhumiwa Festo Maduhu ambaye ni mpenzi wake” imeeleza taarifa hiyo.
MAPYA YAIBUKA DADA WA KAZI ANAEDAIWA KUUAWA NA BOSS WAKE “ALIGOMA KUMZIKA NA ALIMCHUKUA”