Watu watano wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani baada ya gari kubwa la mizigo kuligonga gari dogo aina ya Noah wakati likisubiri kuvuka katika daraja la mchepuko la Kiyegea ambalo lilovunjika mwanzoni mwa mwezi Machi.
Akizungumzia chanzo cha ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa chanzo Cha ajali hiyo ni kufeli kwa breki za roli lililobeba shehena ya cement yenye namba za usajili T233 BXZ na kugonga gari ndogo aina ya Toyota Noah yenye namba za usajili T623 CGY iliyokuwa imebeba abiria kutoka Dumila kuelekea Gairo na kusababisha vifo vya watu wanne hapo hapo na mmoja akifariki wakati akipatiwa matibabu hospitalini.
POLISI YAWAKAMATA WAANDISHI WATATU KWA MADAI YA KWENDA ENEO ALIPOPATIKANA MGONJWA WA CORONA