Club ya Man City ya England imeripotiwa kusikitishwa baada ya kudaiwa kufahamu kuwa Liverpool ni miongoni mwa club za EPL ambazo hazitaki kuona wao wanacheza UEFA Champions League.
Man City waliadhibiwa na FIFA kwa miaka miwili kutoshiriki michuano yoyote ya Ulaya (UEFA Champions League & Europa League) hii ni baada ya kuthibitika kuwa wamevunja sheria ya FFP (Matumizi ya Juu ya Pesa kuliko inachoingiza).
Licha ya Man City kukata rufaa katika Mahakama ya Kimichezo (CAS) lakini club zilizopo Top 10 Ligi Kuu England nje ya Man City wameiomba CAS kuwa Man City asiruhusiwe kushiriki michuano ya Ulaya wakati rufaa yake ikiwa inasikilizwa.
Hii ni baada ya kuwepo kwa dalili zote msimu ujao wa UEFA utaanza rufaa ya Man City ikiwa bado haijatolewa maamuzi, Man City ameshangazwa kuona Liverpool ni miongoni mwa club zilizounga mkono ombi hilo la vilabu vya EPL.
Man City wameshangazwa kwa sababu Liverpool wapo juu yao na uwezekano wa Champions League msimu ujao upo alitegemea kuona vilabu vya chini ndio vinalivalia njuga suala hilo sababu ya kutaka nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya.