Staa wa zamani wa Brazil na FC Barcelona Ronaldinho ataishi katika hoteli ya Palmaroga mjini Asuncion nchini Paraguay wakati huu akiwa nje kwa dhamana ya kesi ya kuingia Paraguay akiwa na Passport bandia.
Ronaldinho ataishi hapo akiwa chini ya uangalizi maalum sababu ya hofu kuwa asije kutoroka baada ya leo akiwa na kaka yake Roberto Assis kuachiwa kwa dhamana ya dola milioni 1.6 (Tsh Bilioni 3.7).
Hotel hiyo yenye hadhi ya nyota nne ambayo Ronaldinho atakaa (presidential suite) kukiwa na bar, Gym na bwawa la kuogelea ili kukaa chumba maalum utalazimika kulipia pound 87 kwa siku (Tsh 249,000/=).