Mamia ya wakazi wa Mkoa wa Arusha hususani wale wanaotokea Wilayani Monduli na maeneo ya jirani, wameshiriki katika ibada maalum ya mazishi ya Mzee Laibon, nyumbani kwake katika Kijiji cha Esilalei, huku wito ukitolewa kwa Wanafamilia na Jamii ya Wafugaji, kumuenzi kwa kudumisha na kuendeleza yale yote aliyo kuwa ameyaanzisha pamoja na yale yote aliyokuwa ameyapanga kuyatekeleza wakati wa uhai wake.