Wakati Duniani nzima ikiendelea na kutafuta tiba na chanjo ya ugonjwa wa Corona, jeshi la wananchi wa Tanzania jwtz, limeendelea na mazoezi ya matumizi ya silaha za kivita huku askari wapya wakiaswa kuzingatia kwa umakini tahadhari zote muhimu katika kujikinga na maambukizi ya Virusi vya ugonjwa huo.
Akizungumza na askari hao wapya katika eneo la msata wilayani bagamoyo mkoani Pwani wakati wa kufunga zoezi la porini Exercise Maliza Kozi ya kuruti kundi la 39 mwaka 2020, mkuu wa mafunzo na utendaji kivita jwtz, Meje jenerali Alfred Kapinga amewaasa askari hao wapya kuzingatia maelekezo yote ya jeshi pamoja na wizara ya Afya ili kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi RTS kihangaiko Canali Sijaona Myala nae akiweka msisitizo juu ya jambo hilo,huku akiwataka askari wote wapya kudumisha nidhamu muda wote wanapokuwa katika vituo vyao, Jumla ya askari wapya 3052 wamehitimu zoezi la porini ambalo lilihusisha kutupa mabomu ya mkono, Matumizi ya rocket ranger,matumizi ya mizinga,vifaru na silaha nyingine za Msaada wakati wa vita.
VIDEO: KATIBU MKUU TFF AIZUNGUMZIA VOICE NOTE YA MANARA KUHUSU KATABAZI