Kanisa Katoliki nchini Burundi limesema limeshuhudia mapungufu mengi wakati wa uchaguzi wa Urais ambayo yanaleta maswali kuhusu matokeo ambayo yametoa ushindi kwa mgombea wa Chama tawala na Chama chake kwa ujumla.
Baraza la Maaskofu Burundi limesema waangalizi waliowekwa katika kila kituo nchini humo walishuhudia masanduku ya kura yakifunguliwa, Maafisa kufanya unyanyasaji na kuwatisha wapiga kura, na Watu kupiga kura katika majina ya watu waliofariki na wakimbizi.
Mkuu wa Baraza la Maaskofu Burundi Askofu Joachim Ntahondereye, amesema zoezi la kuhesabu kura kwenye uchaguzi wa Urais Nchini humo lilifanyika kwa siri na Watu walioidhinishwa waliingia na kutoka kutoka katika vyumba vya kuhesabu kura.
Hii imeandikwa na Idhaa ya Kiswahili
ULIIKOSA HII YA SHEKH KIPOZEO AFUNGUKA ‘MWEPESI WA ZINAA NI MWANAMKE, MWEPESI WA KUIBA NI MWANAUME’