Jeshi la polisi mkoani mkoani Morogoro limetoa siku mbili kwa wenyeviti wa vijiji vitano vilivyopo katika wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kujisalimisha katika kituo cha polisi baada ya vijiji vyao kuthibitika kulima bhangi kwa Zaidi ya hekari 100.
Ni zaidi ya Km 30 kutoka eneo la makazi hapa kijiji cha Misengele Tarafa ya Doma, hadi kufika eneo hilo ulipo Mto Mgeta, kinacho onekana hapa ni umbali kutumika kama fursa kuwawezesha wakazi wa humo kuendeleza kilimo cha Bangi ambapo Mkuu wa Kituo kikubwa cha Polisi mkoani humo ametoa siku mbili kwa viongozi wa vijiji vitano vilivyopo ndani ya kata hiyo kujisalimisha kituoni kwa kutotoa taarifa za uwepo wa mashamba hayo.