Mkutano Mkuu wa CCM umempitisha Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa tiketi ya CCM kwa kura 1,822 za wajumbe sawa na asilimia mia moja ya Kura zilizopigwa na hakuna Kura zilizoharibika.
Akitangaza matokeo ya kura hizo mmoja wa wasimamizi wa uchaguzi ambaye ni Spika wa Bunge Job Ndugai amesema idadi ya wajumbe waliohudhuri ni 1822 na hakuna kura iliyoharibika hivyo ameshinda kwa asilimia 100.