Kutoka India, Mfalme wa kiwanda cha Bollywood Amitabh Bachchan na Mwanae ambaye pia ni Star wa Movie za Kihindi Abshishek Bachchan wamethibitisha kuwa wana virusi vya corona na wamelazwa Hospitali kwa matibabu.
”Mimi na Baba wote tumelazwa Nanavati Mumbai, ambao walikuwa karibu na sisi siku 10 zilizopita wote wapime corona” Abshishek Bachchan
Nae Star wa Movie za Kihindi Aishwarya Rai (Mke wa Abshishek Bachchan) ambaye pia anashikilia Taji la Miss Dunia 1994 na Mwanae wa kike Aaradhya mwenye umri wa miaka 8 wote wamethibitika kuwa na corona na wamejitenga nyumbani kwao,
Abhishek Bachchan na Baba yake Mfalme wa kiwanda cha Bollywood Amitabh Bachchan nao pia wana corona na wamelazwa Hospitali Nanavati Mumbai.