Wizara ya sheria Marekani imesema kwamba aliyekuwa Rais wa Gambia Yahya Jammeh alitumia pesa alizopata kwa njia ya ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma kununua jumba la kifahari huko Washington alipokuwa madarakani.
Kulingana na nyaraka zilizowasilishwa kama sehemu ya juhudi za kutwaa jengo hilo katika Mji Mkuu wa Marekani, Jammeh alinunua jumba hilo lenye thamani ya Dola Milioni 3.5 za Marekani sawa na na zaidi ya Bilioni sabini za Kitanzania miaka 10 iliyopita.
Inasemekana kwamba alinunua jumba hilo kupitia Mke wake Zineb Jammeh.
Jammeh alitoroka Nchi baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa 2017 na sasa hivi anaishi nchini Equatorial Guinea.