Leo July 20, 2020 AyoTV inakukutanisha na kijana Zuberi Ismail mwenye miaka 20 mkazi wa Kigoma ambaye aliishia darasa la 6 na alibuni pikipiki ndogo ya kwanza ambayo ilikua inawaka japo ilikua haina uwezo wa kubeba abiria.
Baada ya Serikali kuona ubunifu huo iliamua kumsomesha Chuo VETA Kigoma ufundi wa magari, leo kaja na ubunifu mwingine wa gari linalotumia ATM Card kama funguo ya kuliwasha.
“Hii gari inatumia ATM card tu, ukiweka kitambulisho haifanyia kazi tunaweza jaribisha ila itagoma, Shule nimesomea umeme wa magari kwa miezi mitatu, hii gari ina kompyuta yake ambayo hapa nimeifanya simu kuwa kompyuta yake” Zuberi