Leo July 20, 2020 kutoka Ilala DSM Waziri wa Nchi, Muungano na Mazingira, Mussa Azzan Zungu amepata kura 148 katika kura za maoni katika Jimbo la Ilala akifuatiwa na Sophia Mjema aliyepata kura 105.
Kwa matokeo haya Zungu anaweza kupata nafasi ya kuendelea kutetea nafasi ya Ubunge kwa jimbo la Ilala katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Ikumbukwe Sophia Mjema ndie aliekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala akaachia na kwenda kutia nia.