Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli leo July 22,2020 akizindua jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi amesema atatoa ushirikiano kwa Vyama vyote vya kisiasa nchini.
“Kampeni za Uchaguzi zitafunguliwa August 26 hadi 27 October, 2020, na uchaguzi utafanyika October 28,2020 itakuwa Jumatano, kwahiyo siku ya Uchaguzi itakuwa ni ya mapumziko tutaitangaza rasmi” -Rais Magufuli
“Tufanye kampeni zetu kwa kuzingatia utaifa, sisi ni wamoja, Wananchi wachague kwa sera zetu sio sera za matusi, mimi ni mwenzenu na nitatoa ushirikiano kwa vyama vyote” Rais Magufuli
“Naipongeza sana Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kwa kujenga jengo lake, tangu mwaka 1993 ilipoundwa haikuwahi kuwa na ofisi yake bali ilikuwa ikiishi kwenye ofisi za kupanga” – Rais Magufuli
“Tunakuombea Mwenyekiti wa NEC Jaji Kaijage pamoja na wenzio mkafanye maamuzi kwa kumtanguliza Mungu ili matokeo mtakayoyatangaza yawe yamezingatia Sheria na maadili, Mungu aibariki Tume ya Uchaguzi, aubariki Uchaguzi Mkuu na awabariki Wanasiasa wote watakaoshiriki Uchaguzi” Rais Magufuli