Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inakaa kikao leo kwa ajili ya kutoa mapendekezo yao kuhusiana na wagombea wa Urais kwa Tanzania Bara na Zanzibar baada ya kufanya utafiti juu ya wagombea hao.
Msemaji wa Chama hicho Tumaini Makene ameeleza kuwa mapendekezo yatakayo tolewa na kikao hicho kwa mujibu wa katiba ya chama hicho yatawasilishwa kwenye kikao cha Baraza Kuu kitakachofanyika kesho Agosti 3, 2020.
“Kamati kuu inakaa kuandaa kwa mujibu wa katiba ya chama kamati kuu inafanya utafiti wa majina ya wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar kupitia Kamati Kuu Zanzibar itaanda ajenda kwa ajili ya kupeleka mapendekezo kwenye kikao cha Baraza Kuu” Makene