Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Prof. Kabudi ameziomba nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kuendelea kuitumia lugha adhimu ya Kiswahili katika shughuli zao za kila siku pamoja na kuiweka katika mitaala yao ya masomo shuleni.
Tukio hilo limehudhuriwa na Mawaziri na viongozi mbalimbali wa Jumuiya hiyo katika mkutano wa 40 wa wakuu wa nchi na serikali wa SADC kwa njia ya kimtandao ikifanyika hivi kutokana na janga la corona ambayo limeikumba dunia.
Kwa upande wake Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania akibainisha namna wanavyojindaa kubeba jukumu hilo la ungozi wa SADC baada ya Tanzania kumaliza kipindi chake.
Zoezi hili la kukabidhi kijiti limeanza tangu Agosti 10, 2020 na litahitimishwa na Rais Dkt John Magufuli Agosti 17 Jijini Dodoma ambaye ndiye kwa mwaka mzima alikuwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa mwaka mmoja tangu Agostit 20 mwaka 2019 akikabidhi kijiti hicho kwa Rais wa Msumbiji.