Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila ameuvunja Uongozi wa Madereva wa Matipa katika Jiji la Mbeya na kuagiza uongozi huo ukamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, baada ya kuweka mgomo wa kusafirisha mawe na hivyo kutoa adha kwa watumiaji na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni tano kwa Serikali kwa kushindwa kukusanya mapato.
RC Chalamila ametembelea eneo linalotumika kuchimba mawe na kuzungumza na wachimbaji ili kujua changamoto ambayo imesababisha madereva wa tipa kugoma kuendelea na biashara ya mawe.
Madereva wa tipa katika Jiji la Mbeya wameaanza mgomo wa kufanya biashara ya mawe tangu August Nane hadi sasa na hivyo kutoa adha kubwa kwa Wananchi wnaohitaji huduma hiyo lakini pia kuikosesha Serikali mapato.