Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, amevitaka vyama vya siasa kufanya kampeni za amani na utulivu katika kipindi chote cha Uchaguzi na baada ya Uchaguzi kwa kile alichodai kuwa kuna maisha baada ya Uchaguzi hivyo hawatakiwi kuvunja amani.
IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo August 19,2020 katika mkutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wadau wa Uchaguzi pamoja na vyama vya siasa, ambao ametaka kila mtu atimize wajibu wake, na kuonya vyama kutoingilia majukumu ya Jeshi la Polisi.
“Msiingilie kazi ambazo sio zenu, baadhi ya wagombea kutangaza dhana ya kulinda kura ambayo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu” IGP Sirro
“Tuko vizuri sana kushughulika na wahalifu, mwanasiasa akijiingiza kwenye uhalifu basi huyo ni halali yetu, hakikisheni mnafanya siasa safi za amani na utulivu” IGP Sirro