Jeshi la kujenga Taifa {JKT} limetangaza nafasi za kujiunga na Jeshi hilo kwa kujitolea kwa vijana wote wa Tanzania Bara na visiwani huku likisisitiza kuwa halihusiki na kuwatafutia ajira vijana pale wanapomaliza mafunzo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa Tawi la Utawala Kanali Julius Kadawi kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Charles Mbuge amesema utaratibu wa vijana kuomba kujiunga na kuchaguliwa na mafunzo hayo utaratibiwa na ofisi za Wakuu wa Wilaya na wakuu wa Mikoa ambapo mwombaji anaishi.
“Jeshi la kujenga Taifa linapenda kuwataarifu vijana kuwa watakaopata fursa hiyo kuwa halitoi ajira kwa vijana na pia halihusiki na kuwatafutia vijana ajira katika asasi, vyombo vya ulinzi na usalama na mashirika mbalimbali serikali na yasiyo ya serikari bali hutoa mafunzo ambayo yatawasaidia vijana kujiajiri wenyewe mara tu wanapomaliza mkataba wao pale tu wanapomaliza mafunzo yao ya Jeshi la kujenga Taifa” Kanali Kadawi
“Sifa za mwombaji awe raia wa Tanzania elimu na umri, vijana wenye elimu ya darasa la saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18 na kwa vijana wenye elimu ya kidato cha nne umri usiwe zaidi ya miaka 20 na kwa vijana wa kidato cha sita umri usiwe chini ya miaka 18″ Kanali Kadawi
“Usiwe zaidi ya miaka 22 vijana wenye elimu ya stashahada umri usiwe zaidi ya miaka 25 na elimu ya shahada usiwe zaidi ya miaka 26, na shahada ya uzamili usiwe zaidi ya 30, na shahada ya uzamivu umri usiwe zaidi ya miaka 35” Kanali Kadawi