Mbrazil Ronaldinho Gaucho ametoka kizuizini alipokuwa anashikiliwa kwa zaidi ya miezi 5 baada ya Mahakama nchini Paraguay kumhukumu adhabu hiyo baada ya kukutwa na hati bandia ya kusafiria.
Staa huyo wa zamani wa vilabu vya PSG, Barcelona na hata AC Milan, alikuwa anashikiliwa na mamlaka za usalama za Paraguay pamoja na kaka yake ,Roberto de Asas ambaye anatambulika kama meneja wa nyota huyu wa zamani.
Nje ya soka Gaucho anatajwa kama mchezaji anayependa sana anasa na maisha ya ufahari yaliyochangia kutofanikiwa zaidi katika soka na hata sakata hili la kuingia nchini Paraguay kwa hati ya bandia inaelezwa kuwa walikuwa wanakwenda katika uzinduzi wa moja ya kumbi za starehe ya usiku maarufu kama Cassino.