Watu watano wamefariki dunia papo hapo katika ajali iliyohusisha gari ndogo lililogongana na basi dogo la Kampuni ya NBS katika Kijiji cha Nyasamba Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga barabara ya Shinyanga Mwanza.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba ambaye amefika eneo la tukio amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari dogo aina ya Toyota Secced kukosa mwelekeo na kugonga basi dogo aina ya TATA, mali ya Kampuni ya NBS lililokuwa likitoka jijini Mwanza kuelekea mkoani Tabora.
“Gari lenye namba za usajili T571 BPZ aina ya Tata Mini Bus ikiendeshwa na Kazimili Maganga likitokea Mwanza kwenda Tabora lilipofika eneo la Nyasamba liligongana na gari jingine dogo likitokea Dar es salaam likiendeshwa na Ramadhan Silaji na kusababisha vifo vya watu watano” Kamanda Magiligimba
“Chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa madereva wa magari yote mawili na uzembe wa dereva dogo ambapo alihama upande wa kushoto na kuendeshea kulia zaidi na kwenda kugongana na basi hilo dogo na kusababisha vifo vya watu watano” Kamanda Magiligimba