Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza siku ya kitaifa ya maombi kwa ajili ya Covid-19 itakayofanyika Jumamosi Agosti 29, 2020.
Amesema wazo la kufanya hivyo amelipata kutoka kwa raia wa Uganda ambaye alikuwa na ‘Maono kutoka kwa Mungu’.
“Kuna Mtu amenifuata na kuniambia Mungu kamuambia kwenye maono kwamba ninapaswa kuandaa maombi ya kitaifa ili Mungu atuepushe na corona, kwahiyo natangaza kuwa August 29,2020 ni siku ya maombi ya Kitaifa na pia itakuwa siku ya mapumziko, baki nyumbani kwako na uombe” Museveni
Hadi sasa Uganda imerekodi watu 2,679 wenye maambukizi ya virusi vya coronana na vifo 28.
KONDAKTA ASIMULIA AJALI ILIYOUA WATU 5 “GARI YAKE ILIHAMA NJIA”