Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye ni mgombea Urais wa Tanzania, Prof. Ibrahim Lipumba amesema Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kisipewe madaraka kwani hakina sifa ya kuongoza nchi
Amesema CHADEMA inapaswa kijitafakari kwa Mgombea waliyemsimamisha inawezekana baada ya kupata ajali amepata matatizo ya akili kwani hoja alizozitoa Tume ya Uchaguzi dhidi yake hazina mashiko
Prof. Lipumba “Sisi tunasimama kusimamia Demokrasia lakini cha ajabu CHADEMA inaniwekea pingamizi, hii ni dhahiri hoja zangu hawaziwezi kwanini waniwekee pingamizi mimi. Kama CHADEMA wapo vizuri basi washindane kwa hoja na sio kuweka pingamizi zisizo na maana kwani hii haijengi demokrasia ya kweli”.