Kampeni za Uchaguzi Mkuu zikiwa zinaanza leo maeneo mbalimbali ya Taifa letu, madereva bajaji na bodaboda wameonywa kuhusu kujiingiza katika maandamano yasiyo na vibali vya Polisi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Morogoro Wilbroad Mutafungwa amesema hivi karibuni kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanasiasa kuwarubuni madereva na kuwaingiza katika maandamano yasiyo na vibali.
“Hakikisheni hamshiriki katika maandamano ya kisiasa ambayo hayana kibali maalumu kutoka Polisi kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria kwa sababu watawanunulia mafuta lita moja kisha mkajiingiza katika vitendo vya uvunjifu wa sheria” RPC Mutafungwa
Amewataka madereva hao kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria na kuhakikisha hawajiingizi katika vitendo vinavyopelekea uvunjifu wa amani.
TUNDU LISSU AMUIBUA PROF.LIPUMBA “ANGEZUIA NISIGOMBEE URAIS, MIMI MPINGO”