Msemaji wa serikali ya Ujerumani amesema mkosoaji wa rais wa Urusi Vladmir Putin ambae mpaka hivi sasa hana fahamu na anapatiwa matibabu mjini Berlin, alipewa sumu inayosababisha kuua mishipa ya fahamu.
Msemaji wa Serikali, Steffen Seibert amesema uchunguzi uliofanyika katika sampuli yake ya damu, kupitia maabara ya kijeshi ya Ujerumani umeonesha ushahidi usio na mashaka kabisa.
Serikali ya shirikisho itatoa taarifa kwa washirika wake wa Umoja wa Ulaya na NATO kufuatia matokeo ya uchunguzi huo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la RIA limemnukuu Msemaji wa Serikali ya Urusi, akisema Ujerumani haijatoa taarifa, kwamba inaamini kuwa Navalny amepewa sumu.
MAJAMBAZI 7 WATEKA GARI LENYE ABRIA 11 ”WAMEPORA MILION MOJA NA SIMU NANE”