Jeshi la Polisi la Mkoani Morogoro inawashikilia watu 3 akiwemo mmiliki wa basi la Kampuni ya HBD, Ahmedi Hemed (25), kwa tuhuma za kuchoma moto basi hilo na kusingizia kuwa moto ulitokana na matatizo ya mfumo wa breki.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, amesema watuhumiwa hao walikula njama ya kufanya tukio hilo baada ya mmiliki kushindwa kulipa deni la basi hilo kwa moja ya taasisi za fedha nchini linalodaiwa kufikia zaidi ya Tsh. Milioni 200.