Kijana Msiba Manyama (18) Mkazi wa Chumwi Wilaya ya Musoma Vijijini katika Mkoa wa Mara anaomba msaada wa mikono bandia baada kupata ajali ya umeme mkubwa uliopelekea ulemavu wa mikono yote na mguu mmoja.
Akipiga story na AyoTV amesema kuwa kutokuwa na mikono ya ziada kunampa wakati mgumu kwani hawezi fanya lolote isipokuwa kufanyiwa kila kitu ikiwemo kufanyiwa usafi wa kimwili na wazazi wake ikiwemo kupelekwa chooni na kuogeshwa.
“Hali hii inanifedhehesha sana maana nakoswa uhuru wa kufanaya mambo yangu naweza mtuma mtu au mzazi maji ya kunywa akaenda ila ukimwangalia vizuri na ukifiria unajua hajapenda na anaona kama ni usumbufu,” Manyama.
Aidha ameeleza kuwa kutokana na hali ya kukaa tu nyumbani bila kazi na anazidi kukuwa na itafika wakati kujiingiza kwenye mahusiano ila ana shaka na huyo mtu atakayemkubali mpaka amuoe kutokana na wasichana wa siku hizi wanaweza mfanyia vituko na kumdharau kisa yeye ni mlemavu., Musiba Manyama
Tel:0718594069