Ni gereza la Sanganer, lililopo katika Mji wa Jaipur nchini India, wafungwa hupewa mahali pa kulala lakini hawapewi chakula na fedha hivyo ni lazima watoke asubuhi kwenda kufanya kazi na kurudi jioni ili wapate kipato kwa ajili ya mahitaji ya kila siku.
Baadhi ya kazi wanazopata wafungwa hao ni kama vile vibarua, kazi za viwandani, udereva na hata ualimu wa yoga, gereza hili halina maeneo ya kuwazuia kutoka nje, halina walinzi katika lango lake kuu na wafungwa huruhusiwa kwenda Mjini na kutafuta kazi.
Ili kufungwa katika Gereza la Sanganer ni lazima uwe umehudumia theluthi mbili za kifungo chako katika Gereza la Kawaida.
Gereza hilo limekuwa wazi tangu 1950 na ni nyumbani kwa wafungwa 450, pia ni miongoni mwa magereza 30 yenye utaratibu huu katika Jimbo la Rajasthan.
Smita Chakraburtty mwanamke anayeoongoza kampeni za kuyafanya magereza yaonekane kuwa mahali pa kawaida, amewasilisha ombi katika Mahakama ya Juu ya India ili kufungua Taasisi zaidi kama hizo.
KIJANA ALIEKATWA MIKONO NA MIGUU NA SHOTI YA UMEME