Li Hua ni raia wa China ambaye anatajwa kama binadamu aliyefanyiwa upasuaji wa hatari zaidi kwa kutenganisha mifupa ya mwili wake ambayo ulijikunja kwa kuelekea mbele kitaalamu ikiitwa Ankylosing Spondylitis.
Li Hua alizaliwa mwaka 1990 katika kijiji cha Yongzhou Kusini mwa China na alipofika miaka 18 alianza kupata matatizo ya kiafya ikiwemo maumivu ya mgongo, nyonga na shingo ambapo tatizo lilikuwa polepole na alipofika miaka 19 viungo vyake vilianza kujikunja kuelekea mbele.
Li Hua alifanyiwa Oparesheni June 2019 na Oparesheni ya mwisho ilikamilika Desemba 2019, ambapo alikaa kwenye uangalizi maalum na ilipofika Septemba 2020 aliruhusiwa rasmi kutoka Hospitali akiwa ana uwezo wa kutembea kama Binadamu wengine.