Wahamiaji haramu 32 raia wa Burundi wamekamatwa Mkoani Tabora wakitokea Mkoa wa Kigoma kuelekea Mikoa ya DSM na Mbeya katika upekuzi watatu wamekutwa na vitambulishio vya kupigia kura vya Tanzania na sita wakiwa na barua za utambulisho kutoka kwa Watendaji wa Kata za Mkoa wa Kigoma na DSM.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habaria Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Amiru Sadick Salim amesema Wahamiaji 25 kati yao wamekamatwa Wilayani Urambo wakiwa ndani ya treni kutoka Kigoma kwenda DSM huku wengine saba kituo kikuu cha mabasi Tabora wakitoka Kigoma kuelekea Mbeya.
https://youtu.be/1CEz9bPn3a4