“Nikipata nafasi Suala la kitandawili kwa wakuliima wa korosho kwa muda mrefu litaisha Nitahakikisha pembejeo bora zinapatikana kwa wakati, kupatikana kwa masoko yasioingiliwa na Utawala” Mgombea Urais Bi Queen Cuthbert Sendiga akiongea na wananchi wa Wilaya ya Lindi, Kijiji cha Mtama
Kupitia Ilani yetu juu ya kuendesha Uchumi wa Kijiditali; manunuzi yatakua ya kidigitali ambapo kutakuwa na ushindani wa wazi upatikanani wa pembejeo kwa wakati na bei muafaka itawezekana ni uboreshaji wa mfumo tu” Mgombea Urais ADC
“Bei ya korosho itakuwa wazi hivyo wakulima watapatiwa fursa ya kuuza korosho yao ama kuitia ushirika au kwa wanunuzi moja kwa moja ili mradi wameshindwa zabuni ya wazi na wakulima kupitia vyama vyao wameridhika” Mgombea Urais ADC
ADC itatathmini upya makato na kodi gandamizi wanayokatwa wakulima ili kuona kama inatija au laa wauza bidhaa nyingine hawaingiliwi kati kwa nini wakulima na mazao yao waingiliwe na kupangiwa bei?” Mgombea Urais ADC