Ni mara ngapi unasikia Wazazi au Watu flani kwenye sherehe ya Ndoa wakisema tumekuzawadia Mtoto wetu zawadi hii leo? inawezekana hili limefanyika sana kimakosa kwa miaka na miaka bila Watu kujua, hata mimi sikuwa nafahamu ndio maana nimeamua kuwafahamisha Watu ili tusifanye makosa tena kuanzia harusi ijayo..
Unaambiwa kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971 kifungu cha 58, Mtu anapotoa zawadi kwenye harusi kisha akataja jina la Mwanandoa mmoja wakati wa utoaji basi zawadi hiyo itakua halali kwa huyo Mwanandoa mmoja pekee na sio Wanandoa wote.
Mwanasheria Hamza Jabir kutoka Avis Legal anasema kama lengo ni kuwazawadia Wanandoa wote, Mtoaji anatakiwa kuwataja wote >> “Mzazi akimtaja Mwanandoa mmoja mfano Jane nakupa mali hii au zawadi hii….. basi zawadi hizo zitakua mali ya Mtu mmoja alietajwa ambae ni Jane, haya ni mambo ya kuzingatia Wazazi kama wanataka kuzawadia Wanandoa wote wanatakiwa kutaja majina ya wawili hao”
KUTANA NA BEATRICE, MUUZA KEKI MWENYE MASTERS MBILI