Tume ya Uchaguzi Uganda imempitisha Mbunge wa Kyadondo na Mwanamuziki Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine kugombea Urais wa Nchi hiyo.
Baada ya risiti zake kukaguliwa, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Justice Simon Byabakama amesema “Tumethibitisha stakabadhi zilizowasilishwa na mgombea kwamba ametimiza vigezo vyote vya uteuzi.”
Bobi Wine pia alikumbushwa na Tume kwamba mikusanyiko ya umma bado imepigwa marufuku na kwamba kampeni zake zote zitaendeshwa kulingana na miongozo ya Tume ya Uchaguzi.
Bobi amenukuliwa akisema “huu ni mwanzo mzuri kuelekea kuiokomboa Uganda, nimekuja kumsaidia kazi Mzee wangu Museveni ambaye amekaa Ikulu kwa miaka 34 tangu mwaka 1986″
Bobi atachuana na Rais Yoweri Museveni kwenye kuwania Urais wa Uganda kwenye uchaguzi wa mwaka 2021.