Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeziasa nchi na watu wote kuwa makini katika matumizi yao kwani athari za kiuchumi zilizosababishwa na janga la corona au COVID-19 hazijaisha na zitaendelea kwa muda.
Kwa mujibu wa IMF mgogoro wa kiuchumi uliosababishwa na COVID-19 utaacha majeraha ya muda mrefu katika maisha ya watu kuanzia kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira na kufungwa kwa shule.
Aidha itapelekea kushuka kwa thamani ya fedha kutokana na watu na makampuni kufilisika na changamoto kubwa katika sera za siku zijazo kutokana na nchi kuwa na mzigo mkubwa wa madeni huku makundi ya waliokuwa hatarini na masikini sasa kutumbukia katika ufukara zaidi.
UWEZO WA KOMANDO WA JWTZ, UTABAKI MDOMO WAZI