Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kushirikiana na na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Zipora Liana imesema imefuatilia utekelezaji wa mradi wa stendi mpya ya mabasi mbezi na kufanikiwa kudhibiti zaidi ya shilingi bilioni 12 .
Akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za TAKUKURU Mkurugenzi Mkuu Jenerali John Mbungo amesema fedha hizo ambazo zimedhibitiwa zingeweza kulipwa kwa wakandarasi kama ziada kwa kazi ambayo haijafanyika.
“Uthibiti huu umefanyika kwa kuwa wachunguzi na wataalamu wa ujenzi kutoka TAKUKURU wamekuwa wakifuatilia kazi hii kwa karibu“Jenerali John Mbungo
Aidha Jenerali Mbungo amekabidhi fedha kwa Mkaguzi wa idara ya ukaguzi wa ndani Rehema Mkumbwa kutoka Shirika moja la kimataifa lisilo la Kiserikali kiasi cha shilingi milioni 118, ambazo zilichepushwa kwa njia ya udanganyifu kutoka katika shirika hilo.
Katika hatua nyingine Takukuru inawashikilia watumishi wa nne wa mfuko wa taifa wa bima ya afya nhif kwa mahojiano kwa ubadhilifu wa fedha kiasi Cha shillingi za kitanzania million 500.4 ambapo hatua za kisheria zitachkuliwa kwa watakaothibitika.