Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewatahadharisha Wafanyabiashara kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali ila pia kuwafutia vibali Wawekezaji au Wafanyabiashara watakaoonyesha dalili za usumbufu wa kulipa Kodi kwa biashara wanazoendesha nchini.
Bodi ya Mapato Zanzibar ‘ZRB’ imesema zaidi ya Shilingi Bilioni 17 zinadaiwa kutoka kwa wafanyabiahsara wa miradi mikubwa na wamiliki wa hoteli.
Ni ziara fupi aliyoifanya katika ofisi hiyo ya ukusanyaji wa mapato ya Zanzibar ZRB, iliyolenga kuangalia utendaji kazi wa ofisi hiyo muhimu ndani ya Nchi inayohataji maendeleo yakiuchumi.
Akizungumza na watendaji wa ofisi hiyo Makamu wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdallah ameomba kupatiwa majina ya wafanyabiashara wote wanayodaiwa na bodi hiyo.
Kwa kuwa mamlaka ya ukusanyaji wa mapato Zanzibar ndio yenye jukumu la kusimamia mapato ya Serikali Makamu wa Pili akawahimiza watendaji hao kuhakikisha uweledi na nidhamu ya kazi ndio unawaongoza katika majukumu yao ya kila siku wawapo kazini.