Mashindano ya mpira wa miguu kwa wavulana chini ya umri wa miaka 20 yaliyoandaliwa na shirikisho la mpira wa miguu Afrika Mashariki (CECAFA) ikishirikisha nchi tisa yanatarajia kuanza kufanyika mkoani Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Idd Kimanta amesema hadi sasa nchi mbili zimeshawasili kwa ajili yakujiandaa na mashindano hayo ambapo mechi hizo zitachezwa katika viwanja viwili vilivyochaguliwa ikiwemo cha Sheikh Amri Abeid Stadium pamoja na kiwanja cha Black Rhino.