Waziri wa Uchumi wa Bluu na Uvuvi Abdallah Hussein Kombo amesema endapo Zanzibar itajikita zaidi kwenye uchumi wa buluu kupitia shughuli za uvuvi visiwani hapa utasaidia kukuza ajira na kukuza uchumi wa Zanzibar.
Waziri huyo alitekeleza miongoni mwa maagizo aliyoyatoa Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi kuhusu kukutana na wadau wa sekta ya uvuvi wakiwemo kampuni ya uvuvi ya Salmini na wavuvi.
Waziri huyo amesema Serikali ya awamu ya nane imeamua kujikita kwenye uchumi wa bluu ambapo tayari imeonyesha ishara nzuri mpaka sasa.
“Kampuni ya uvuvi ya Salmini imepata soko la samaki aina ya jodari nchini Finland,Uturuki na China ambapo kila mwezi wanatakiwa samaki tani 5,000 hivyo kampuni hiyo imepanga kununua samaki kwa wavuvi wadogo visiwani Zanzibar” Waziri Kombo