Meneja Mawasiliano wa EWURA, Titus Kaguo, amesema mtu anapokwenda kujaza mafuta anapaswa kuhakikisha kwenye pampu inasomeka alama 00 ndipo aanze kujaziwa mafuta, vinginevyo anaweza kuibiwa.
“Mfano kama kuna mtu kapita hapo kajaza mafuta ya 20,000 na wewe umepita unataka kujaza pengine 50,000 hakikisha alama zile kwenye pampu zinasomeka ‘00’ kwa sababu usipohakiki utajaziwa kwa kuanzia ile 20,000 aliyojaziwa mwenzako,” Kaguo
Amesema ili kuepuka usumbufu kama huo ni vyema wenye magari wakaachana na kawaida ya kubaki kwenye magari wakiendelea na mambo mengine kwa kuwa hali hiyo inatoa mwanya wa kuibiwa na watumishi wa aina hiyo.
Amesema ili uanze kujaziwa mafuta hakikisha mkono wa pampu umerudi kwenye sehemu yake ya kawaida na hesabu isome 00.
“Kama mkono wa pampu haujarudi kwenye sehemu yake ya kawaida inamaana akikuwekea mafuta unaweza kukuta hesabu inaanzia ile ambayo mwenzako aliyepita amewekewa,” Kaguo