Mwanamke mmoja katika mji wa Marion kusini mwa Adelaide, Asutralia alishtuka kutoka usingizini saa kumi na moja alfajiri kufuatia kusikia harufu ya chakula iliyokuwa ukitoka jikoni kwake.
Baada ya kwenda jikoni alimkuta mwanamke aliyeingia nyumbani kwake bila taarifa akikaanga mayai na kuku.
Mwanamke huyu mvamizi mwenye umri wa miaka 43 aliondoka nyumbani hapo bila usumbufu wowote, lakini aliondoka na pakti ya sigara aliyochukua kutoka kwenye nyumba hiyo.
Mwenye nyumba aliwapigia simu polisi na walimkamata mwanamke huyuo akiwa anatembea barabarani, na sasa anasubiri kufikishwa mahakamani kwa kosa la wizi, na amekataliwa dhamana.