Serikali imeongeza muda wa mwaka mmoja kwa Hospitali ya Huruma iliyopo Wilayani Rombo kuendelea kutoka huduma kama hospitali teule ya Wilaya kwa ajili ya kusubiri kukamili kwa ujenzi wa hospitali teule ya Wilaya inayojengwa tarafa ya Useri.
Naibu Waziri wa Afya Dr. Godwin Mollel amefikia uamuzi huo akiwa kwenye ziara ya kikazi kwenye Jimbo la Rombo baada ya kupokea maombi ya Mbunge wa Jimbo hilo Prof. Adolf Mkenda aliyeiomba Serikali kusitisha maamuzi yake ya kuindoa hospitali hiyo kutoa huduma kama hospitali teule ya Wilaya ifikapo Julai mwakani.
Mbunge wa Jimbo la Rombo ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda amesema ujenzi wa hospitali teule ya Wilaya inayojengwa tarafa ya Useri itakuwa rahisi kuwahudumia wakazi wa tarafa za Useri,Tarakea na Masharti ambapo wanaotoka tarafa za Mengwe na Mkuu Pamoja na masharti itawawia vigumu kutokana na Geografia ya eneo hilo.