Rais wa Marekani, Donald Trump amerekodiwa akimwambia Afisa Mkuu wa Uchaguzi jimbo la Georgia atafute kura za kutosha kuwezesha kubadilishwa kwa matokeo ya uchaguzi.
“Nataka tu kupata kura 11,780,” amenukuliwa Trump akimwambia Katibu wa Chama cha Republican, Brad Raffensperger jimboni humo katika mazungumzo yaliyorekodiwa na kutolewa na gazeti la Washington Post.
Katika mazungumzo hayo, Raffensperger anasikika akijibu kuwa matokeo ya uchaguzi ya Georgia yalikuwa sawa.
Rais mteule, Joe Biden alishinda uchaguzi wa Georgia pamoja na majimbo mengine muhimu na kumuwezesha kupata kura 306 za wajumbe dhidi ya Trump aliyepata kura 232.
Tangu uchaguzi mkuu wa Novemba 3, Trump amekuwa akidai kuwa kura ziliibwa bila kutoa ushahidi wowote unaothibitisha madai yake.
Tayari majimbo yote 50 yamethibitisha matokeo ya uchaguzi huo baadhi ya vituo ikiwa ni baada ya kura kuhesabiwa tena au pia kwa sababu ya kesi zilizowasilishwa mahakamani kupinga matokeo.
Bunge linatarajiwa kuidhinisha rasmi matokeo ya uchaguzi huo Jumatano ya Januari 6.
“INJINIA NIKUKUTE POLISI” MOTO WA NAIBU WAZIRI APIGA SIMU PAPO HAPO