Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetolea ufafanuzi taarifa juu ya kupanda kwa gharama za kodi za magari yaliyotumika yanayoingia nchini baada ya Wafanyabiashara ya magari kulalamika.
TRA imesema, ushuru hutozwa kutokana na umri wa gari ambao hufuata mwaka wa kalenda. Magari madogo yenye umri wa miaka nane hadi tisa hutozwa ushuru wa bidhaa wa 15% na zaidi ya hapo hutozwa 30%.
Hivyo ushuru unaonekana kupanda kwa kuwa kuna walioagiza magari yenye miaka tisa mwaka 2020 lakini yameanza kuingia nchini mwaka 2021 hivyo wanalipa ushuru 30%.
TRA imesema, uthaminishaji wa bidhaa hufanyika kwa mujibu wa Kifungu cha Sheria ya Forodha ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 iliyorejewa mwaka 2019 kikisomwa pamoja na jedwali la nne la Sheria hiyo.