IGP wa Uganda, Martin Okoth Ochola amekanusha taarifa kuwa Polisi huwalenga Waandishi wanaofuatilia Uchaguzi, akisema Vikosi vya Usalama hutumia nguvu ili kuwalinda Wanahabari.
Amesema wamekuwa wakiwaambia Waandishi baadhi ya maeneo sio salama na hawatakiwi kwenda, hivyo wanalazimika kuwapiga kwa usalama wao na hawawezi kuomba radhi kwa hilo.
Kauli ya IGP imekuja baada ya Mwandishi mmoja kuuliza kama Polisi wana mpango wa kuomba radhi kwa kilichotokea Desemba 27, 2020 ambapo Waandishi watatu walipigwa na Polisi Wilayani Masaka.
Ochola amesema sio kama Polisi huwalenga Waandishi, bali Waandishi huwalenga Polisi kwa kuonesha ni wakatili na kwamba wanaitetea Serikali.