Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uganda, Jenerali Jeje Odongo amesema, anashindwa kueleza mahali walipopelekwa watu waliochukuliwa na Wanajeshi kipindi cha Uchaguzi Mkuu.
Waandishi wa Habari waliuliza kwa kutaja majina ya watu kumi ambao walikamatwa na wanajeshi wakiwa nyumbani kwao au maeneo ya kazi.
Waziri alisema kuwa, hawana ripoti za watu kupotea hata hivyo alisema namna nzuri ya kusaidia ni kutaja gari, mahali na siku ambayo watu hao walikamatwa.
LIVE: JPM “NATUMA MESEJI KWA WAZIRI WA AFYA, KATIBU NA WATENDAJI, KWANINI MADAWA HAYAPATIKANI?