Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imejifunza kuwa inapotangaza hadharani kuhusu kupandishwa mishahara, kumekuwa kunatengeneza gharama kubwa na kusababisha ugumu wa maisha ya wengine.
Ameeleza hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Konde (ACT-Wazalendo) Khatib Haji aliyehoji ni lini Wafanyakazi wa Tanzania watapandishiwa mishahara na kuboreshewa maslahi
Waziri Mkuu amesema, “Eneo la Wafanyakazi peke yake ukitangaza hadharani kwamba tumepandisha mishahara kwenye masoko, vituo vya mabasi na huduma nyingine zote zinapanda”
Amekiri ni kweli wafanyakazi wengi wanasubiri kusikia kupanda kwa mishahara akisema hilo likifanyika linatengeneza ugumu wa maisha, hivyo bado Serikali inaendelea kutafuta njia nzuri ya kuongeza maslahi ya mtumishi.
Aidha, Waziri Mkuu ameeleza kuwa maslahi ya wafanyakazi hayapo kwenye mishahara tu bali pia kwa kuwapandisha daraja na kupunguza kiwango cha kodi.
MREMBO MDOGO MUUZA SAMAKI, ANAINGIZA MAMILIONI “NALIMA MPAKA NALALA SHAMBA, NIMEAJIRI”